0
Rais John Pombe Magufuli leo September 25, 2016 ameungana na waumini wa kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano wakati wa Ibada ya Jumapili katika kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 katika Pentekoste.
Rais JPM amezungumza na waumini wa kanisa hilo na kuwashukuru kwa kuungana na madhehebu mengine katika kuliombea amani Taifa. JPM aliyeongozana na mkewe Janeth Magufuli katika ibada hiyo amesema madhehebu yote yamekua na kazi kubwa na muhimu katika taifa na kwamba watanzania wote bila kujali dini zao, itikadi za kisiasa, makundi na kanda zao wana wajibu wa kuungana na viongozi wa dini katika kuombea na kulinda amani.
>>>Ninawashukuru kwasababu mnaendelea kuliombea taifa hili, ninawashukuru kwasababu kila siku mmekuwa mkipiga magoti na kumtanguliza Mungu mbele, ninawashukuru kwakuwa mnaendelea kuombea amani ya nchi yetu na upendo udumu ndani yetu sote.
Makanisa yote, dini zote, madhehebu yote, vyama vyote upendo tukiujenga ndio tutaiendeleza vizuri tanzania yetu:- Rais JPM
Katika ibada hiyo Rais JPM alitoa shilingi milioni moja kwaajili ya kuchangia vikundi vya kwaya vya kanisa hilo.

Post a Comment

 
Top