Septemba 25 2016 ilikuwa ni siku
ambayo wabunge wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walicheza mchezo wa
hisani kwa ajili ya kukusanya fedha za watu waliopata na tetemeko la
maafa Bukoba, wabunge walijigawa katika timu mbili wale wabunge ambao
wanaishangilia Yanga na wabunge wa Simba.
Mashabiki ambao walikuwa wamejitokeza
uwanjani kuangalia wabunge hao wakiwa katika mavazi ya timu
wanazozishabikiwa mbunge na waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu
Nchemba alikuwa ni miongoni mwa wabunge waliowanyanyasa wabunge wa Simba
kwa kuwaonesha uwezo mkubwa katika kuuchezea na kumiliki mpira.
Hata hivyo katika mchezo huo ambao
waziri Mwigulu aliifungia magoli mawili timu ya timu ya wabunge wa Yanga
kati ya ushindi wa goli 5-2, waziri Mwigulu alionekana kuwasumbua
baadhi ya wabunge kwa kupiga chenga, hadi dakika 90 zinamalizika wabunge
wa Yanga waliondoka na ushindi wa goli 5-2.
Magoli ya wabunge wa Yanga yalifungwa na
Jadal Hamisi dakika ya 4, Musa Sima dakika ya 5, Hamidu Bolali dakika
ya 9 na mwisho Mwigulu Nchemba akahitimisha kwa kufunga magoli mawili ya
mwisho na kuwafanya wabunge wa Yanga kuondoka na Kombe la Ubingwa wa
mchezo huo wa Hisani.
Post a Comment