0
Septemba 30 2016 wakala wa mchezaji ghali zaidi duniani Mino Raiola ameweka wazi kwa nini kocha wa Man United Jose Mourinho alishindwa kumsajili Paul Pogba wakati akiwa Chelsea, Raiola ameweka wazi kuwa Mourinho ni miongoni mwa makocha waliokuwa wanamuhitaji Pogba kwa muda mrefu.
Raiola ameeleza kuwa kilichomfanya Jose Mourinho amkose Paul Pogba akiwa Chelsea, kwa sababu alikuwa na makubaliano maalum na klabu ya Juventus kuhusu kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa, Raiola alikuwa ameshaubaliana na Juventus kuwa Pogba aisaidie timu hiyo kutwaa taji la Serie A na UEFA Champions League ndio aondoke.
az2zgmjz0lfghcpn4xmdoxojbzmtt2bj
Mino Raiola
“Pogba angeweza kuondoka Juventus mwaka uliopita kwa sababu Jose Mourinho alimuhitaji wakati yupo Chelsea, kiukweli alimuhitaji sana lakini Juventus na mimi tulikuwa na makubaliano kuwa aisaidie timu kutwaa taji la Serie A na Champions League kwanza ndio angeweza kuruhusiwa kuondoka” >>>> Raiola

Post a Comment

 
Top