0
 
Baada ya Diamond Platnumz kutajwa kuwania tuzo  za MTV MAMA 2016 zinazotolewa na kituo cha TV cha MTV Base Africa, sasa Tuzo nyingi zinazidi kutambua juhudi na kazi yake kwenye muziki wa Tanzania ambapo good news ni kwamba amepata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania kwenye tuzo za Ghana Music Awards UK.
Tuzo za Ghana Music Awards UK zinazoandaliwa kwa ushirikiano wa kampuni mbili za Alordia Promotion & West Coast UK Entertainment za nchini Ghana na Uingereza.
Diamond Platnumz anawania tuzo hii kupitia kipengele cha AFRICAN ARTIST OF THE YEAR akichuana na mastaa wengine akiwemo Patoranking, Fally Ipupa, Davido, AKA, Wizkid, Olamide na Tekno Milles.
Sherehe za utoaji wa tuzo hizi zimepangwa kufanyika jijini London, Uingereza mnano November 5 2016.

Post a Comment

 
Top