Suala la
unywaji wa pombe ni jambo la kawaida, lakini matumizi ya kinywaji hicho
yakizidi kiwango yanaweza kukuaibisha mtu wangi. Ni kawaida pia siku
hizi kupita maeneo mengi na kukuta watu wakiwa wanakunywa pombe ikiwa
kama moja ya starehe muhimu kwa watu wengi.
Nimeipata
hii kutoka nchini Kenya kuhusu Utafiti uliofanywa nchini humo kuonesha
kuwa, watu wenye kipato cha juu ndio hunywa pombe kwa kiasi kikubwa na
kila panapokuwa na wanaume saba kwenye Bar, kuna mwanamke pia.
Kwa mujibu wa utafiti huu uliofanywa na
wizara ya afya nchini Kenya, umeongeza kuwa raia milioni 6 wa Kenya ni
wanywaji waliopindukia wa vilevi.
Utafiti
huu umeonesha kuwa, miongoni mwao watu ambao huwa wanafurahia kunywa
vilevi, asilimia 24 ni watu matajiri na asilimia 18 ni watu masikini au
wenye kipato cha chini, huku asilimia 50 kati yao, sio masikini wala
matajiri.
Matokeo ya
utafiti huu yametokana na mahojiano yaliyofanywa face to face na
wahojiwa elfu 45 wenye umri wa kati ya miaka 18 na 69. Licha
ya kuwa utafiti huu ulilenga kutoa mwanga kuhusu uhusiano kati ya
watumiaji wa vilevi na magonjwa ya kuambukiza, umeonesha pia asilimia 13
ya Wakenya wameathiriwa na ulevi na hawawezi kuacha kunywa.
Hata hivyo
asilimia ya watu wanaotumia vilevi hatari huenda ikawa ni kubwa zaidi
hata kufikia asilimia 36 na idadi kubwa ya watu hawa wanapatikana kwenye
maeneo ya vijijini ambako pombe hizi kupatikana kwa wingi. Utafiti huu umekuwa ni wa kwanza kufanyika nchini Kenya kuhusu magonjwa yasiyoambukiza. Daktari
Gladwell Gathecha kutoka kitengo cha magonjwa yasiyoambukiza kwenye
wizara ya afya, amesema kuwa, lengo lilikuwa ni kubainik hatari
zinazowakabili watumiaji wa vilevi na mazingira yanayoweza kuwasababisha
kupata maambukizik ya magonjwa, ili waweze kuandaa mpango wa kuzuia.
Utafiti
umeonesha kuwa kwa sehemu kubwa watumiaji wa vilevi wamekuwa wakipata
maambukizi yanayoweza kuepukika kutokana na kutotumia mboga za majani na
matunda. Ni asilimia 6 tu ya Wakenya ndio wenye uwezo wa kupata vitamini kutoka kwenye mlo kamili, huku asilimia 94 hawana uwezo huo.
Utafiti
huo pia umeongeza kuwa asilimia 84 ya Wakenya hupendelea kuongeza chumvi
na Sukari nyingi wakati wa uandaaji wa chakula majumbani mwao.
Post a Comment