0
Akiongea na Ayo TV kwa niaba ya Vodacom Tanzania ambao ndio wadhamni wakuu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo,Nandi Mwiyombella, amesema wakiwa kama wadhamini wakuu wa ligi ya Vodacom Tanzania bara.
Vodacom wanazitakia kila la kheri timu za Yanga na Simba katika mzunguko wa kwanza kwa timu hizi kubwa hapa nyumbani  zitakazomenyana siku ya jumamosi ya tarehe 1 mwezi Oktoba katika uwanja wa Taifa jijini Da res Salaam, mchezo huo utakuwa mzuri na wakuburudisha washabiki wote wa timu hizi watakaofika uwanjani kuushuhudia kwani ni mara ya kwanza kwa timu hizi kukutana tangia msimu huu kuanza.
Kwa mashabiki watakaoshindwa kwenda uwanjani Vodacom Tanzania haitawaacha mbali na matokeo yatakayokuwa yakiendelea uwanjani hapo”LIVE” ili kupata matokeo ya mchezo huo ni rahisi sana unachotakiwa kufanya ni kujiunga na kifurushi cha ‘Soka bando’ na utakuwa unapata fursa ya kupata matokeo kiurahisi kabisa popote pale ulipo ya timu yako uipendayo.
Kifurushi hichi ni chenye gharama nafuu ya shilingi 500/-ni mahususi kwa ajili ya mashabiki wa mchezo wa mpira wa miguu unaopendwa duniani kote kinawapatia mashabiki wa soka muda wa maongezi wa dakika 14 Vodacom kwenda Vodacom na pia dakika 2 vodacom kwenda mitandao mingine, na pia utapata sms 20 kwa masaa 24.
Kununua kifurushi cha soka bando anachotakiwa kufanya mteja ni kupiga  namba *149 * 01#, Ofa mpya halafu chagua ‘Soka Bando’. Baada ya  hapo mteja atapata ujumbe unaomtaka ajisajili kwa timu ya soka anayoishabikia kwa kutuma jina la timu mfano “Yanga”  “Simba” au “Azam” nk. kwenda namba 15460.Pia mteja anaweza kupata taarifa za soka kupitia tovuti ya  Mspoti.vodacom.co.tz.

Post a Comment

 
Top