1.Ipo taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikimnukuu Waziri wa
Nchi -Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) Mhe.
Angellah J. Kairuki (Mb), kuwa Serikali itaanza kutoa ajira, kupandisha Vyeo na
kulipa Stahiki mbalimbali za Watumishi wa Umma mwezi Februari, 2017. Chanzo cha
habari hiyo ni mtandao wa Jamii Forum kupitia mjadala ulioanzishwa na nkanga chief (JF-Expert Member) na baadaye kusambazwa
katika mitandao mingine.
2.
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inapenda
kuwafahamisha Watumishi wa Umma na Umma kwa ujumla kuwa, taarifa hiyo haina
ukweli wowote na ina lengo la kuupotosha
Umma. Hivyo watumishi wa
umma na wananchi kwa ujumla wanaombwa kuipuuza taarifa hiyo na kuendelea na majukumu
yao kama kawaida.
3.Serikali inasisitiza
kuwa, suala la Ajira mpya na upandishaji Vyeo litafanyika kwa kuzingatia Bajeti
ya Serikali ya Mwaka wa Fedha 2016/17. Malipo ya stahili
za watumishi wa umma yatafanywa na Serikali kwa kuzingatia, Sheria, Kanuni na
Taratibu zilizopo.
4. Ikumbukwe, Serikali ina utaratibu maalum wa kutoa taarifa kwa Umma,
hivyo Serikali itatoa taarifa rasmi kwa Umma kupitia mamlaka husika.
5. Serikali kupitia taarifa
hii inawaasa wananchi kuacha tabia ya kusambaza habari za uongo au
zisizothibitishwa dhidi yake. Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria
wale wote watakaobainika kuzusha na kusambaza habari za upotoshaji kuhusu
shughuli za Serikali.
Imetolewa na:
Post a Comment