Matumla alipokelewa katika chumba cha wagonjwa wa dharura MOI jana alfajiri tarehe 06/02/2017 akiwa na maumivu makali ya kichwa na hali ya kupoteza kumbukumbu na fahamu na baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina pamoja na kupata vipimo mbalimbali ikiwemo vya CT-SCAN ya ubongo ambapo kulibainika kuwa amepata jeraha kichwani na kwenye ubongo ambalo limepelekea damu kuvilia kwenye ubongo kitaalamu (Acute subdural hematoma) na kusababisha mgandamizo kwenye ubongo upande wa kulia ambapo alihitaji upasuaji wa haraka na wa dharura.
Baada ya vipimo jana saa 3 asubuhi Matumla aliingizwa katika chumba cha upasuaji kwa ajili ya upasuaji mkubwa wa ubongo (craniotomy)na kuondoa damu iliyovilia kichwani na upasuaji huo ulifanyika kwa mafanikio makubwa na ulifanywa na jopo la wataalamu wetu wazalendo 5 kwa muda wa masaa 3 na tumejiridhisha kuwa ameondolewa kwenye hatari ya kupoteza maisha.
Taasisi ya MOI inapenda kuwataarifu watanzania na wapenzi wa mchezo wa ndondi kwamba Matumla ataweza kurudi katika hali yake ya kawaida katika kipindi cha miezi 8 hadi 12 ambapo ataweza kucheza mchezo wa ngumi baada ya kupata kibali maalumu cha daktari.
IMETOLEWA NA KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI MOI DR,OTHMAN KILOLOMA 7TH FEBRUARY 2017
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.