Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo
Januari 23, 2018 ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa halmashauri ya
Butiama mkoani Mara Solomoni Ngiliule kuanzia leo kutokana na ubadhirifu
wa fedha za Umma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo ametangaza maamuzi
hayo leo zikiwa zimepita siku tatu toka Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
alipotoa maagizo kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bw. Raphael
Nyanda kutuma timu ya wakaguzi kwenda kufanya ukaguzi maalumu katika
ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Butiama.
Waziri Mkuu aliagiza kiongozi huyo kuchunguzwa kutokana na matumizi
yasiyoeleweka ya fedha za miradi ya maendeleo zinazotolewa na Serikali
zikiwemo sh. milioni 12 walizotumia kuandaa profile ya Halmashauri hiyo
huku fedha zingine ni pamoja na sh. milioni 70 za elimu maalumu, sh.
milioni 288 za mradi wa maji Butiama ambazo zote hazikujulikani
zimetumikaje.
Post a Comment