Polisi
nchini Maldives imemkamata Jaji Mkuu wa Mahakama ya Juu nchini humo
huku mgogoro wa kisiasa ukiendelea kuwa katika hali mbaya kwenye nchi
hiyo iliyoko katika bahari ta Hindi.
Jaji
Mkuu Abdulla Saeed na Jaji Ali Hameed, walikamatwa na polisi baada ya
nchi hiyo kutangaza hali ya hatari huku kukiwa hakuna maelezo
yaliyotolewa na uchunguzi au mabadiliko juu ya mtafaruku huo ulipata
kasi baada ya rais wa nchi hiyo Abdulla Yameen alipokataa kutii amri ya
Mahakama ya kuwaachilia wafungwa wote wa kisiasa.
Maldives
ni taifa dogo katika bahari ya Hindi likiviunganisha visiwa vidogo
1,192 na utalii ndiyo chanzo kikubwa cha mapato ya nchi hiyo. Wiki
iliyopita Mahakama ya juu nchini humo iliamuru kuachiwa kwa wanasiasa wa
upinzani na pia Mahakama hiyo iliamua kwamba mashitaka ya rais wa
zamani wa nchi hiyo Mohamed Nasheed ya mwaka 2005 ambaye yuko uhamishoni
yalikuwa kinyume na katiba.
Hatua
hiyo ya Mahakama ya juu ilifuatiwa na tamko la Kamishna Mkuu wa Jeshi
la Polisi ambaye alisema kuwa atatekekeleza amri ya Mahakama na mara
baada ya kauli hiyo kamishna huyo alifukuzwa kazi na Rais Adulla Yameen
huku jeshi la nchi hiyo likiamuriwa kukataa kumuondoa Rais Yameen
madarakani.
Post a Comment