Wakati Simba na Yanga zikipaa kueleka Djibout na Shelisheli kucheza michezo yao ya Kimataifa, wadau mbalimbali wa soka wamejitokeza na kuwakumbusha kubeba bendera ya Taifa na kuweka mbele uzalendo.
Winga wa zamani wa Simba, Ulimboka Mwakingwe anasema Simba na Yanga, zinaenda kuwakilisha taifa, hivyo utani wa jadi baina yao, usihusike kimataifa kwa kuwataka wachezaji wa klabu hizo watangulize utaifa.
"Tushindane kwa ligi ya ndani,tunapocheza na mataifa mengine, tubadilike kuanzia wachezaji hadi mashabiki kuziombea na kuziunga mkono, ili hata wakija kucheza uwanja wa nyumbani wasipate mpenyo wa kushinda,"anasema.
Staa wa zamani wa Yanga, Sekilojo Chambua anasema neno utaifa likifanyia kazi kwa Watanzania ndipo hatua katika soka zitapatikana akisisitiza kwamba hakuna haja kuweka utofauti wakati hizo klabu zinawajibika kuwakilisha nchi.
"Upinzani wa ndani usiingilie pale Simba na Yanga,zinaposhiriki michuano ya kimataifa,tuziombee kwa pamoja ili ziweze kupeperusha bendera ya taifa vema kama vile tunavyowaombea watu wa riadha,"anasema.

Post a Comment