0

Big Boss wa Cash Money Records, Birdman amemmwagia sifa rapa Nicki Minaj na kusema kuwa ndiye rapa bora wa kike kwa sasa.

Birdman ametoa sifa hizo kwa Nicki na kusema kuwa ni ‘Best female in hip hop’ wakati wa mahojianao aliyokuwa akifanya na jarida la Rap-Up  hivi karibuni.

“I always say she’s the best ever, best female ever in hip-hop, hands down, facts. There’s no getting around it. There’s levels to this s**t. Very much levels to this s**t. She’s an elite.”

Mkali huyo pia hakusita kumuongezea sifa mrembo huyo anayesumbua katika muziki wa Hip Hop na kusema kuwa unaweza ukamueka Nicki katika chumba na wanaume wanao-rap lakini yeye atakuwa noma zaidi.

Hata hivyo baadhi ya watu wakiwemo Djs wameonekana kumponda rapa huyo wa kike akiwemo Dj Funk Master Flex wa Hot 97 ambaye amemuita Nicki #WACK.

Post a Comment

 
Top