0

Mshambuliaji wa Yanga, Mzimbabwe, Donald Ngoma, anatarajiwa kuanza mazoezi na kikosi cha timu hiyo kesho Jumatatu.

Kwa mujibu wa kauli ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika, alisema taarifa alizozipata kutoka kwa Daktari wa timu, Edward Bavu, mchezaji huyo yupo fiti kuanza mazoezi Jumatatu ya kesho.

Nyika alitoa kauli hiyo mapema baada ya Yanga kuwasili ikitokea Botswana kushiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers FC.

Ngoma atakuwa anarejea uwanjani akitokea kwenye majeraha ya nyonga aliyoyapata tangu Agosti, mwaka jana kutokana na tatizo hilo na kulazimika kukaa nje ya uwanja akiuguza maumivu hayo.

Post a Comment

 
Top