0
Mwanamitindo wa kiume hapa bongo maarufu kwa jina la Brown, ambaye alikuwa mpenzi wa Wolper, ametua kwenye mikono ya muigizaji mwengine wa Bongo Movie Salma Jabu maarufu kama Nisha.

Wawili hao wameonekana kuweka picha za kimahaba pamoja kwenye mitandao yao ya kijamii, huku moja ikiwa imenadikwa juu ya kufutwa kwa tatto ya jina la Wolper ambaye alikuwa mpenzi wa zamani wa Brown, kabla hawajamwagana.

Www.eatv.tv ilimtafuta Nisha bebe kujua kama kweli wawili hao ni wapenzi baada ya mrembo huyo kuwahi kusema kuwa hataki tena kuwa kwenye mahusiano na viben ten, na kukimbia kujibu suala hilo.

:Nitakujibu baadae sasa hivi nipo na watu wengi”, alisikika Nisha akimjibu reporter wa www.eatv.tv kuhusu kuwa kwenye mahusiano na Brown.

Kitendo cha Nisha kuwa na Brown kimeonekana kama kujichoresha kwani mara nyingi mrembo huyo akiweka wazi mahusiano yake huishia kumwaga machozi insta, baada ya kukimbiwa.

Alichopost Nisha Instagram


Post a Comment

 
Top