Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) halijakaa kimya kipindi hiki ambacho msanii wa Bongo Fleva Ommy Dimpoz anaumwa.
Kupitia ukurasa wao wa mtandao wa Twitter wamemtakia msanii huyo afya njema kipindi hiki anapatiwa matibabu nchini Afrika Kusini.
"THREAD: Imeripotiwa tena msanii na ndugu yetu @ommydimpoz amerejea hospitalini kwa matibabu zaidi. Tunasimama na wapenda sanaa, wapenzi wake na watanzania wote kwa ujumla katika kumwombea na hatimaye arejee katika afya yake."
Tangu mwezi mwaka huu Juni Ommy Dimpoz amekuwa akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini ambapo alifanyiwa upasuaji wa koo kisha baadaye alirejea nchini na sasa amerudishwa tena Afrika Kusini.
Post a Comment