Siku
chache baada ya kuondoka star Trey Songz aliyekuja Afrika Mashariki
katika nchi ya Kenya kwenye msimu wa Coke Studio Afrika unaofanyika
jijini Nairobi, Hii ni good news tena kwako shabiki wa muziki wa R&B
kutoka kwa star wa single ya Sexy U Back To Sleep Chris Brown
amethibitisha kuwa ataingia nchini Kenya mwezi ujao.Star
huyo wa muziki wa Hip Hop na R&B atafanya show yake ya kwanza nchi
Kenya katika ukumbi wa Mombasa Golf Club wiki ijayo, October 8, 2016.
Tamasha hilo litawakutanisha wasanii ambao kwasasa wamekua marafiki
zaidi, Wizkid kutoka Nigeria atakayepanda steji moja na Chris Breezy
just imagine itakuaje mtu wangu. Chris Brown amecomfirm kuja kwake
Afrika Mashariki kupitia Video fupi iliyopostiwa kwenye mtandao wa
YouTube, akiwataka Wakenya wajitokeze kwa wingi siku hiyo. “Yoyo
001, Mombasa Kenya, can’t wait to come out there. Kenya we are turning
it up. October 8th make sure you’re there, make sure you’re ready and we
are gonna party, thank you,” anasikika mshindi huyo wa tuzo ya Grammy Award. Wakenya watapata nafasi ya kumshuhidia
Breezy kwenye stage kwa kiingilia cha shilingi 10,000 za Kenya kwa
tiketi za kawaida huku VIP ikiwa shilingi 20,000 na VVIP itakua shilingi
50,000 za Kenya.
Post a Comment