Leo September 29, 2016 Taasisi ya Twaweza
wamefanya uzinduzi wa ripoti ya utafiti mpya jijini Dar es salaam.
Utafiti huo unaeleza kuwa Watanzania wengi hawaoni kama nchi inaendeshwa
kidikteta baada ya mtu mmoja kati ya 10 waliohojiwa kueleza nchi
inaongozwa kwa mfumo huo.
Matokeo ya utafiti huo uliofanywa kwa njia ya simu kati ya Septemba 24-29
mwaka yanasema kuwa watu sita kati ya 10 sawa na asilimia 58 walipinga
kuwa nchi inaongozwa kidikteta huku asilimia 31 wakieleza kutokuwa na
uhakika. Katika utafiti huo unaoitwa “Demokrasia, udikteta na
maandamano: wananchi wanasemaje”, mwananchi mmoja kati ya watatu
alitafsiri udikteta kuwa ni kitendo cha Serikali kutumia nguvu wakati wa
kuitawala nchi.
Licha ya wananchi wengi kueleza hawaoni nchi ikiongozwa kidikteta, ripoti hiyo iliyohoji watu 1,602
wa Tanzania Bara inaeleza kuwa wananchi saba kati ya 10 wanaunga mkono
demokrasia kama mfumo bora wa Serikali, mtazamo ambao unaoshabihiana na
wafuasi wa vyama mbalimbali nchini.
Pamoja na kuhoji masuala mbalimbali namna nchi inavyoendeshwa, Twaweza
walihoji watu pia ufuasi wao kwa vyama vya siasa ambapo asilimia 66
walieleza kuwa karibu na CCM huku asilimia 19 wakiwa karibu na upinzani
hususan Chadema. Watu wawili kati ya 10 (asilimia 15) walisema hawana
ukaribu na chama chochote.
Post a Comment