Mahakama
ya Wilaya ya Ilala imemhukumu kifungo cha maisha jela, Erick Kasila
(39) baada ya kupatikana na hatia katika mashtaka matatu likiwamo la
kumlawiti mwanamume kwa madai kuwa alimfumania gesti na akiwa na mke
wake.
Kasila
anadaiwa kumlawiti Idd Kambi katika nyumba ya kulala Wageni ya Maembe,
Yombo Kiwalani, Wilaya ya Ilala na kumpiga picha za utupu na kutisha
kunitumia katika mitandao ya kijamiina kumnyang’anya nguo alizovaa,
fedha, laptop na viatu.
Mshtakiwa
wa pili katika kesi hiyo, Juma Richard (31) alihukumiwa kifungo cha
miaka 14 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlazimisha mlalamikaji
kumnyonya uume wake na kumtaka kusaini karatasi ya ahadi ya Sh1 milioni
ili asisambaze picha walizompiga wakati wakimlawiti, ambazo hata hivyo,
walizisambaza katika mitandao ya kijamii.
Akisoma
hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Said Mkasiwa
alisema ameridhishwa na ushahidi wa mashahidi watano dhidi ya washtakiwa
na vielelezo vya picha zinazoonyesha mlalamikaji alikuwa analawitiwa,
nyingine zikionyesha mshtakiwa akimlazimisha mlalamikaji amnyonye sehemu
zake za siri.
Akipitia
baadhi ya ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, Hakimu Mkasiwa alisema
kulawitiwa kwa mwanamume huyo ni baada ya kukutwa na Sanifa Bakari
ambaye ni mke wa Kasila.
Kabla
ya hukumu hiyo, upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali,
Silvia Mitanto uliiomba Mahakama kutoa adhabu kali dhidi ya washtakiwa
hao kwa kitendo walichokifanya ambacho kimemuathiri mlalamikaji
kisaikolojia.
Washtakiwa walipopewa nafasi ya kujitetea kwa nini wasipewe adhabu kali, walishindwa na badala yake waliomba nakala ya hukumu.
Post a Comment