Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kimetekeleza agizo la Rais John Magufuli ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho la kuwalipa mishahara na haki zao
nyingine zinazofikia Sh milioni 609 wafanyakazi wa Kampuni ya Uhuru
Publications (UPL) wanaozalisha magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani.
Rais
Magufuli alitoa agizo hilo mwezi uliopita alipofanya ziara ya ghafla
katika ofisi ya magazeti hayo na kusikiliza malalamiko ya wafanyakazi na
baadaye kuagiza ndani ya mwezi huo, wafanyakazi walipwe mishahara na
haki zao zote.
Msemaji
wa chama hicho, Christopher ole Sendeka akizungumza na waandishi wa
habari Dar es Salaam jana alisema pia miongoni mwa maagizo ya Rais
Magufuli ni kutaka wafanyakazi hao kutobughudhiwa wala kufukuzwa kazi
baada ya kueleza changamoto zinazowakabili na kuhakikisha wanalipwa haki
zao.
“Nataka
kuwahakikishia mpaka hapa tunapozungumza sasa hivi hatudaiwi
tumeishatekeleza maagizo ya Mwenyekiti, tuko safi labda katika sehemu
nyingine,” alisema.
Katika
ziara hiyo, Rais Magufuli aliagiza kupatiwa orodha ya taasisi za
serikali zinazodaiwa na Magazeti ya Uhuru na Mzalendo, na pia aliagiza
kulipwa kwa deni linalodaiwa na Shirika la Hifadhi ya Jamii la NSSF
kutokana na kutowasilishwa kwa makato ya wafanyakazi.
Katika
mazungumzo yao na Rais, wafanyakazi walilalamikia kutolipwa mishahara
yao kwa miezi saba, kutowasilishwa kwa michango ya wafanyakazi kwa NSSF,
kuuzwa kwa mtambo wa kuchapisha magazeti katika hali ya kutatanisha,
kutotambuliwa katika ajira kwa baadhi ya wafanyakazi, kutolipwa kwa
madeni wanayozidai taasisi za serikali na wanaostaafu kutolipwa mafao
yao.
Post a Comment