0

Mti  wa  ukwaju. Majani yake hutumika  katika  tiba  ya  kuongeza  maziwa  kwa  mama  anaye nyonyesha.
Tiba   Ya   Miguu   Kuwaka  Moto
:

1.   Chukua  majani  ya  mti  wa  Mvumbasi, unguza  pamoja  na majani ya  mti  wa  mnungunungu, halafu changanya na  mafuta  ya  taa  lita  moja. Matumizi:  Utakuwa unatumia  kujichua kwenye  miguu  kutwa  mara  tatu  kwa  muda  wa  siku  thelathini. Utapata  nafuu  kubwa  sana.
Tunda  la  topetope;Mizizi ya  mtopetope hutumika  katika  tiba  ya  kuondoa  uvimbe  kwenye  kizazi.
2.     TIBA   YA  KIKOHOZI: Tafuna  majani  ya  mti wa mbaazi. Mbali  na  kutibu  kikohozi, mti  wa mbaazi, unatibu  magonjwa mengine  mengi.  Mfano, mizizi ya  mti wa  mmbaazi, husaidia  kutibu  chango la  kiume  na  kusafisha kibofu cha  mkojo.
 
3.   KUVIMBA  KWA  TEZI LA  SHINGO:  Kama una  sumbuliwa  na  tatizo  la  tezi kuvimba, chukua  unga  wa  Kamun Nyeusi, kisha  changanya  na sega  la  nyuki, halafu  tumia  kukanda kwenye  tezi, kila  siku  kwa  muda wa mwezi  mmoja. Utapata mafanikio  makubwa  sana.
 
4.   TIBA  YA MAUMIVU  YA  MGONGO, MIGUU, NYONGA NA  KIFUA  KUPASUA:
Kama una  sumbuliwa  na  maumivu  ya  mgongo, miguu, nyonga  na  kifua  kupasuka, fuata  maelekezo  yafuatayo:
Chukua mafuta  ya  nyonyo robo lita, mafuta ya   Kamun Nyeusi kiasi cha robo lita pamoja  na  mafuta ya  karafuu robo  lita , changanya  pamoja  halafu  uwe  unatumia  kujichua  sehemu yenye  maumivu, kutwa  mara tatu  kwa siku  thelathini. Utapata  nafuu  kubwa sana.
 
5.   TIBA  YA  KWIKWI : Kama unasumbuliwa  na  kwikwi, fuata  maelekezo  yafuatayo : Chukua  majani ya  mwembe  mkavu, pekecha  kisha  mpe  mgonjwa  atumie  kuvuta  kama  sigara  halafu awe  anameza moshi.  Tatizo  la  kwikwi  litaisha. 
 
6.    Tatizo  La  Kukojoa  Kitandani ;  Kama  una  tatizo  la  kukojoa  kitandani, tumia mizizi ya  mbaazi  kwa  kuchemsha, na  kunywa  maji  yake  kutwa mara  mbili  kwa  siku, kwa muda wa siku  kumi  na  nne.

7.    Tatizo  la  uvimbe  kwenye  kizazi :  Kama  una  tatizo  la  uvimbe  kwenye  kizazi, chukua  mizizi  ya  mtopetope,  tumia kwa  kuchemsha  na kisha  kunywa  maji  yake, mara  tatu  kutwa  kwa siku  thelathini.
 
8.     Vidonda  vya  koo : Kama una  tatizo  la  vidonda  vya  koo, chukua maji  ya  uvuguvugu kiasi  cha nusu  lita, kisha  kamulia  ndimu  tatu fresh, halafu  tumia  kusukutulia. Utafanya  hivyo  mpaka, utakapo  pata  nafuu.
 
9.   Malaria sugu :  Kama  una  malaria sugu, chukua  maji  ya  dafu  moja, weka  kwenye chombo  kisafi, kisha  kamulia  ndimu  saba, halafu  tumia  kunywa. Fanya  hivyo  mara  mbili  kwa  siku, asubuhi  na  jioni  kwa  siku  tatu hadi  saba. Hakika  utapata  matokeo  mazuri  sana.
 
10.         Tiba  ya  tatizo  la kutoa harufu  mbaya  kinywani, sehemu  za  siri, kikwapa  na  jasho lenye  harufu  mbaya :   Chukua  maji  yaliyo  lowekewa  mchele  kiasi  cha  lita  moja, kisha  tumia  kunawia  sehemu  husika  na  kusukutulia  mdomo. Utafanya  hivyo mara  tatu  kwa  siku  hadi  utakapo  ridhika  na  matokeo  unayo  yahitaji.
 
11.          Kwa wakina  mama; Jinsi yakuzuia uchungu wamimba,maumivu yakiuno, maumivu wakati wahedhi, na damu itokayo bila mpangilio wasiku maalumu,Chukua majani ya mbigili yatwange halafu changanya navijiko vitatu  vikubwa  vya unga wa mti unaitwa msonobali kisha  tumia kunywa glasi 1 yenye  ujazo  wa  milimita  mia  mbili  na  hamsini,  kutwa  mara  tatu hadi  hali yako  itakapokua nzuri
 
12.         Tiba  Ya Vidonda  Vya  Tumbo,Kisukari  pamoja   na  Typhoid:
Chukua mizizi ya mti wa  msongati pamoja na majani ya mkalatusi  vitwange kwa pamoja  kisha  chemsha  kwenye  maji  lita moja,  halafu tumia  kunywa glasi moja ya  robo  lita, mara  tatu kwa  siku  kwa  siku  thelathini. 
 
13.         Tiba  Ya  Tatizo  La  Kukosa  Hamu  Ya  Tendo La  Ndoa  Kwa  Wanawake :   Kama  wewe  ni  mwanamke  unaye  sumbuliwa  na  tatizo  la  kukosa  hamu ya  tendo  la  ndoa,  unaweza  kutibu  tatizo  lako  kwa  kutumia  vyakula  mbalimbali  kama  ifuatavyo :
i.                   JUISI  YA  MIWA :  Tumia  kunywa  nusu lita  hadi  lita  moja  ya  juisi  ya  miwa, mara  tatu  kwa  siku asubuhi, mchana  na  jioni  kwa  siku  thelathini. Utapata  matokeo  mazuri. Mbali  na  kuwasaidia  akina  mama  wenye  tatizo  la  kukosa  hamu  ya  tendo  la  ndoa, juisi  ya  miwa  ina  faida  nyingine  nyingi  kitabibu. Moja kati  ya  faida  kubwa  za  juisi  ya  miwa, ni  uwezo  wake  mkubwa  wa  kusafisha  figo. Hivyo  hata  wanaume  wanashauriwa  kutumia  juisi  ya  miwa  au  miwa  kwa  wingi,kwa  sababu  inasaidia  kusafisha  figo, na  figo  ni  moja  kati  ya  ogani  muhimu  sana  katika  mfumo  wa  nguvu za  kiume.
ii.              MBEGU ZA FENESI : Chukua  mbegu za  fenesi  kiasi  cha  robo kilo,  kisha  chemsha  na  maji lita  mbili, halafu  tumia  kula  pamoja  na  supu yake. Utafanya  hivyo  mara  tatu  kwa  siku kwa  muda  wa  siku  thelathini. Hakika  utapata  matokeo  mazuri  sana.  Unaweza  pia  kuzisaga  na  kutumia  unga  wake, kwa  kuchemsha  na kunywa, kwa  kufuata  utaratibu  huo  hapo  juu.
iii.           KOROSHO : Tumia  kula  korosho  pakti  moja  yenye  ujazo wa  robo  kilo, mara  tatu kwa  siku, asubuhi, mchana  na  jioni  kwa  siku  thelathini. Yaani  asubuhi, tumia  robo kilo, mchana  robo  kilo  na  jioni  robo  kilo kwa siku  thelathini. Utapata  matokeo  mazuri.
iv.            MIHOGO  MIBICHI :  Tumia  kutafuna  walau  vipande  vitatu  vya  mihogo  mibichi  kwa  siku, kwa muda  wa  siku  thelathini. Yaani  asubuhi  utumie  kipande  kimoja  kikubwa,mchana kipande  kimoja  kikubwa  na  usiku, utumie  kipande  kimoja  kikubwa.
 
14.         TIBA  ASILIA  YA  TATIZO  KIFUA KISICHO PONA  KWA  WATOTO  WADOGO WALIO KUNYWA UCHAFU WAKATI WA KUZALIWA, PUMU, KIFUA KISICHO PONA KWA WATU WAZIMA,KICHOMI,KUWASHWA MWILI NA KUPALIWA WAKATI UMELALA USINGIZINI
Tiba  Yake, chukua majani  ya  mpera kiasi  cha kama  viganja  vinne, yaponde  pamoja  na magome  ya  muembe kiasi  cha viganja  vinne, na  tunda  la  koma manga, twanga  vyote  kwa  pamoja  ( Yani majani  ya  mpera, magome  ya  muembe na tunda  moja  la  komamanga ).
Ukisha  maliza  kutwanga, changanya  na  maji  lita mbili  halafu  chemsha  pamoja na lita  moja  ya  asali mbichi  ya  nyuki  wadogo. 
 
Chemsha  hadi  itokote, halafu  ipua  dawa  yako.
 
 Matumizi : Kwa  mtoto  mdogo mwenye  umri wa  kati ya  mwaka  mmoja na  miaka  mitano, tumia  kumpa  kijiko kimoja  kikubwa  mara  mbili kwa  siku, asubuhi  na  jioni n  kwa  siku  saba.
 
Na kwa  mtu mzima, tumia  kunywa  vijiko  vikubwa   viwili  mara  mbili  kwa siku  asubuhi na  jioni, kwa siku  ishirini  na  moja

15.         KUJITIBU  TATIZO LA  MTOTO  WA  JICHO :  Kujitibu  mtoto  wa  jicho, tumia  kunyunyizia  jichoni  matone mawili ya  utomvu  wa toto la  ndizi. Fanya  hivyo  mara  tatu  kwa  siku, asubuhi, mchana  na  jioni kwa  siku  thelathini. Utapata  matokeo mazuri.
 
Mbali  na  kutibu  tatizo  la mtoto  wa  jicho, toto la ndizi, likichanganywa  kitaalamu  na  wine  ya  mnazi ( Palm wine ) au mnazi,  husaidia  kutibu  tatizo  la  kidole  tumbo  au  appendix.
 
16.         TIBA  ASILIA  YA  KUPUNGUZA  GESI TUMBONI
Kuondoa  gesi tumboni, kwa  kutumia  tiba  asilia, chukua juisi ya kitunguu maji kiasi cha glasi moja yenye  ujazo  wa  milimita  mia  mbili  na  hamsini,kisha changanya  na asali mbichi kijiko kimoja  koroga  halafu tumia  kunywa .
Utafanya hivyo  mara tatu kwa siku kwa  muda  wa  siku  kumi  na  nne.
 
AU  chukua  kipande  kimoja  cha  tangawizi,kiponde ponde  kisha  chemsha  kwenye nusu lita ya  maji pamoja  na  kijiko  kimoja kikubwa  cha  asali  mbichi  ya  nyuki wadogo, halafu  tumia kunywa  kutwa  mara  mbili  kwa  siku  ishirini na  moja.
 
AU ; Chukua asali  mbichi  ya  nyuki  wadogo  kiasi  cha  robo  lita,  changanya  na vijiko  vitatu  vikubwa  vya  unga  wa  Kamun nyeusi,kisha chemsha  pamoja  kwenye  maji  lita  moja.Halafu tumia kula  vijiko  vikubwa  vitatu  kutwa  mara  tatu kwa  siku  ishirini  na  moja.
 
17.         TIBA  YA  PUMU :  Chukua magadi vijiko vikubwa  vitatu, saga  upate  unga wake, kisha  changanya  na samli ya  n’gombe   vijiko 21  vikubwa na  asali  vijiko 30 vikubwa. Matumizi : Tumia  kula  vijiko  vikubwa  vitatu  asubuhi, vitatu  jioni na  vitatu  usiku kwa  muda  wa  siku  thelathini.  Utapata  nafuu  kubwa  sana.
 
18.         TIBA  ASILIA  YA  KIHARUSI  NA  KIFAFA :
Chukua mizizi  mitatu  ya  mti  wa  ukwaju, mizizi  mitatu  ya  mti  wa  mkungu, mizizi  mitatu  ya mpapai, pamoja  na  mizizi  mitatu  ya mti  wa  ufwambo.  Iponde  ponde  yote  kisha  chemsha  kwa  pamoja  kwenye  maji  ya  lita tatu  hadi  yachemke. Tumia  kumpa  mgonjwa  glasi  moja, kutwa  mara  tatu kwa  siku  thelathini. Mgonjwa  wako  atapata  nafuu  kubwa  sana.
 
19.         TIBA   ASILIA YA FANGASI ZA   KWENYE DAMU, UKURUTU, UPELE, MCHAFUKO WA DAMU, PAMOJA  NA KUWASHWA  KWA MWILI.
Chemsha  robo  kilo  ya  majani  ya  mti  wa  mdimu kwenye  maji kiasi cha  lita  mbili. Maji yakisha   tokota, ipua  chuja, halafu  tumia  kunywa  glasi mbili  asubuhi, mbili  mchana, mbili  jioni. Utafanya  hivyo  kwa  muda  wa  siku thelathini.  Hakika  utapata  nafuu  kubwa  sana.
 
20.         TIBA   ASILIA  YA  MARADHI YA FANGASI ZA MIGUU NA KUNUKA MIGUU.
Twanga  majani ya  mwarobaini  robo  kilo,  chemsha  na  maji lita  tano, kisha weka  kwenye  beseni  halafu  loweka  miguu  yako ndani  ya  beseni  kwa  muda  wa  lisaa  limoja. Utafanya  hivyo  kutwa  mara  mbili kwa muda  siku  kumi  na  nne. Utapata  matokeo  mazuri sana.
 
AU  chukua majivu kiasi  cha  robo kilo,changanya  na robo  lita ya  juisi  ya  ndimu, kisha  nyunyizia  kwenye  miguu, na ukae kwa  lisaa  limoja. Utafanya  hivyo  mara mbili  kwa siku  kwa  siku  thelathini. Japo inauma  lakini  ni tiba nzuri  sana.

21. KUONGEZA  MAZIWA  KWA  MAMA  ANAE NYONYESHA : Chukua  majani  ya  mti  wa  ukwaju, kiasi  cha nusu kilo, kisha  chemsha  na  maji  lita tano.  Tumia  kunywa glasi  tatu  asubuhi, tatu mchana, tatu  jioni kwa  muda  wa  siku saba.  Hakika  utapata  matokeo  mazuri  sana. Utakuwa  unafanya  hivyo  kila  mara  utakapo  hitaji kuongeza  maziwa. 
 
MAKALA  HAYA  YAMELETWA  KWENU  KWA  HISANI YA  NEEMA  HERBALIST & NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC. DUKA  LA  KUUZA  DAWA  MBALIMBALI  ZA  ASILI.
 
 TUNAPATIKANA  UBUNGO  JIJINI  DAR  ES  SALAAM, JIRANI  NA  SHULE  YA  MSINGI,UBUNGO  NATIONA  HOUSING NYUMA  YA  JENGO  LA  UBUNGO  PLAZA.
 
KWA MAHITAJI  YAKO  YA DAWA  MBALIMBALI  ZA ASILI  ZINAZO  TIBU  MAGONJWA  NA  MATATIZO  MBALIMBALI  YA  KIAFYA, WASILIANA  NASI  KWA  SIMU  NAMBA 0766 53 83 84.
 
NA  KWA  TAARIFA  ZAIDI  KUHUSU HUDUMA  ZETU, TEMBELEA  KILA  SIKU KATIKA  BLOGU YETU.

Post a Comment

 
Top