Chama cha ACT-
Wazalendo kimemuomba Rais John Magufuli kuunda timu ya wataalamu kupitia
upya rasimu ya Katiba ya Jaji Joseph Warioba na kuitisha mkutano mkuu
wa kikatiba ili kuipitisha.
Chama hicho kilisema mchakato wa kura za maoni uanze upya ili kupata Katiba Mpya.
Chama hicho kilisema mchakato wa kura za maoni uanze upya ili kupata Katiba Mpya.
Hayo ni
miongoni mwa maazimio matatu yaliyotolewa na chama hicho kwenye
mkutano wa siku moja wa kidemokrasia.
Akisoma maazimio hayo, Ofisa
Habari wa chama hicho, Abdallah Khamis alisema, “chama kimeazimia
mchakato wa kuandika Katiba Mpya uanze kwa kufanya marekebisho ya sheria
ya kura ya maoni na Sheria ya mchakato wa Katiba.”
Alisema, iwapo
Serikali itaamua kwenda na Katiba Inayopendekezwa iliyopo sasa chama
hicho kitaipinga kwa kufanya kampeni ya hapana kwenye kura ya maoni.
Alisema wakati mchakato wa Katiba ukiwa umesimama, Baraza la Wawakilishi
Zanzibar limepitisha sheria ya kutafuta mafuta na gesi kinyume na matakwa ya
Katiba ya Muungano ambayo inatambua mafuta na gesi kuwa ni masuala ya
muungano.
“Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia umeshauri kuwa chama
kimwelekeze mbunge wake kuwasilisha bungeni hoja binafsi ya kufanya
mabadiliko, kwa kuondoa mafuta na gesi kama jambo la muungano ili
kuiwezesha Zanzibar kutafuta mafuta na gesi asilia bila vikwazo,”
alisema.
Khamis alisema chama hicho kimeazimia kufanya maadhimisho ya
miaka 50 ya Azimio la Arusha Februari, 2017.
“Katika maadhimisho hayo
chama kifanye mkutano mkuu wa Kidemokrasia jijini Arusha na kutanguliwa
na Halmashauri Kuu ya chama kwenye ukumbi uleule ambao Tanu ilifanya na
kuzaa Azimio la Arusha mwaka 1967,” alisema.
Ofisa huyo alisema katika
maadhimisho hayo chama kimeshauriwa kuwa wataalamu wa ndani na nje
waalikwe kujadili mafanikio na changamoto za Azimio la Arusha katika
miaka 25 iliyopita.
Pia, wataalamu watajadili madhara ya kutelekezwa kwa Azimio la Arusha mwaka 1992 huko Zanzibar.
Pia, wataalamu watajadili madhara ya kutelekezwa kwa Azimio la Arusha mwaka 1992 huko Zanzibar.
Post a Comment