Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe
31 Oktoba, 2016 ameondoka nchini kuelekea Nairobi nchini Kenya kwa
ziara ya Kiserikali ya siku mbili nchini humo kwa mwaliko wa Rais wa
Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Rais Magufuli ameagwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mkuu wa Mkoa wa Dar Es salaam, Paul Makonda na viongozi mbalimbali wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Mara
baada ya kuwasili nchini Kenya, Rais Magufuli atafanya mazungumzo rasmi
na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta, na baadae atakwenda kutoa heshima
katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Kenya Hayati Mzee Jomo Kenyatta.
Mheshimiwa Rais pia anatarajiwa kuhudhuria dhifa ya kitaifa atakayoandaliwa na mwenyeji wake Ikulu Jijini Nairobi.
Katika
ziara hiyo Rais Magufuli anatarajiwa kutembelea kiwanda cha maziwa cha
Eldoville kilichopo Karen Jijini Nairobi na pia kuzindua barabara
mchepuko (Southern By-pass) iliyopo Jijini humo. Barabara hiyo ni moja
kati ya miradi mikubwa ya barabara nchini Kenya, inayounganisha maeneo
mbalimbali ya Jiji la Nairobi kwa barabara za juu na chini.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar Es Salaam
31Oktoba, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
akisindikizwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Uwanja
wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa tayari kwa safari ya
kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba
31, 2016. Hii ni safari yake rasmi ya tatu kwenda nje ya nchi toka
aingie madarakani mwaka mmoja uliopita. Alisafiri kwa mara ya kwanza
alikwenda Rwanda, kisha akaenda Uganda.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana
na Naibu Balozi wa Kenya nchini Mhe Boniface Muhia katika Uwanja wa
ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa tayari kwa safari ya kwenda
Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31,
2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea
saluti toka kwa Inspekta jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu katika
Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa tayari kwa safari
ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo
Oktoba 31, 2016
Makamu
wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
John Kijazi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na
viongozi wengine wakipunga mikono kumuaga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere wakati akianza safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa
ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016. PICHA NA IKULU
Post a Comment