Mawaziri
Wakuu wa zamani ambao ni wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa na Frederick Sumaye
wameweka kambi mjini Dodoma ili kuteta na wabunge wa Ukawa.
Mkurugenzi
wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema
alisema kuwa wanasiasa hao wako mjini humo kwa ajili ya kufanya vikao na
wabunge wa Ukawa ili kuweka mkakati na msimamo dhidi ya hoja mbalimbali
zinazotarajiwa kuibuliwa katika vikao vya Bunge vinavyoanza kesho.
Moja
kati ya hoja zinazotarajiwa kuwekewa msimamo ni pamoja na kuupinga
muswada wa huduma za habari unaotarajiwa kujadiliwa na kupitishwa kuwa
sheria.
“Tutakuwa na kikao cha kuweka msimamo wetu dhidi ya muswada hatari wa huduma za habari,” Mrema anakaririwa. “Vikao vimeshaanza na vitaendelea kesho (leo),”aliongeza.
Kwa
mujibu wa Mrema, mbali na Lowassa, Sumaye na mwenyekiti wa Chadema,
Freeman Mbowe, vigogo wengine wa Ukawa waliohudhuria vikao hivyo ni
pamoja na Profesa Mwesiga Baregu, Profesa Abdallah Safari na Arcado
Ntagazwa.
Post a Comment