Kampuni
ya Bia ya Serengeti (SBL) jana imetangaza kuzindua shindano la DJ bora
ambalo linalenga kuibua na kukuza vipaji katika sekta ya muziki na
burudani nchini Tanzania.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa shindano hilo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Serengeti John Wanyancha alisema kuwa shindano hilo
limedhaminiwa na bia inayozalishwa na kampuni hiyo Smirnof Black Ice,
na wakati huo huo ikimaanisha kuwapatia mashabiki wa muziki fursa ya
kufurahia vibao vya muziki vya hivi karibuni vitakavyochezeshwa na
ma-DJ walio na vipaji vikubwa.
Kwa
mujibu wa Wanyancha, Smirnof Black Ice ni chapa inayoongoza katika
vigezo vya bia iliyotayari kunyweka ikiwa ni maarufu mioongoni mwa
wanywaji wa tabaka la kati katika maeneo yote ya mjini na vijijini.
“Tunaamini
kwamba kupitia shindano hili SBL itawapa wakati mzuri wapenzi wa
muziki watakaokuwa wanatembelea baa wakati tukitoa fursa maridhawa ya
kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji katika ulimwengu wa muziki na
ma-DJ."
Mkurugenzi
huyo aliyataja majiji ambayo yatakuwa wenyeji wa matukio na idadi ya
ma-DJ watakaotoa burudani katika mabaa kwenye mabano kuwa ni Dar es
Salaam (20), Dodoma (4), Arusha (5), Morogoro (4), na Mwanza (5).
Shindani hilo linaanza mwezi huu wa Oktoba na litadumu hadi Desemba.
Aidha
Mkurugenzi huyo alisema kuwa hadhira inayolengwa katika mashindano
hayo ni vijana walio na umri kati ya miaka 18 hadi 30 na kufafanua kuwa
burudani hiyo inawafaa sana wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo vingine
vya elimu ya juu pamoja na vijana walio na weledi.
“Itakuwepo zawadi nono kwa ma-DJ watakaoshinda,” alisema
na kubainisha kwamba zawadi hizo zitajumuisha seti ya vifaa vya
kuchanganya muziki, kompyuta mpakato na mashine kuchanganya muziki kwa
washindi watatu watakaoingia fainali.
“Tunatoa
wito kwa ma-DJ wote, wasimamizi wa baa na wapenzi wa muziki katika
majiji haya kushiriki kwa wingi katika shindano hili la kuvutia ili
kufurahia na burudani inayotolewa na sekta ya muziki nchini Tanzania,” alisema Wanyancha.
Post a Comment