Siku
moja baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William
Lukuvi kutangaza nia ya Serikali kumnyang’anya shamba Waziri Mkuu wa
zamani, Frederick Sumaye, mwanasiasa huyo mkongwe amedai hilo
halimtikisi.
Sumaye
ambaye tayari ameshakabidhiwa notisi ya siku 90 kutokana na
kutoliendeleza, amesema kuwa tayari suala hilo ameshaliwasilisha
mahakamani na kwamba mwanasheria wake ndiye anayefahamu tarehe
iliyopangiwa kesi hiyo.
“Nilienda
mahakamani na ikaamuriwa kusiwe na shughuli yoyote, nasubiri tarehe ya
kesi ambayo mwanasheria wangu ndiyo anaijua,” Sumaye anakaririwana
MwanahalisiOnline.
Mwanasiasa
huyo aliyehamia Chadema miezi michache kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi
Mkuu mwaka jana, amesema kuwa kama CCM wanataka kumdhoofisha kwa
kumnyang’anya mashamba ili arejee haitawezekana.
“Kama
walidhani kwa kunifanyia hivi nitarudi Chama Cha Mapinduzi (CCM)
wasahau, hata kama nilikuwa na nia hiyo sirudi,” amesema Sumaye.
Serikali
imetangaza kuanza mchakato wa kumnyang’anya Sumaye shamba lake lililoko
Mwabwepande jijini Dar es Salaam kwa madai kuwa ameshindwa kuliendeleza
kwa muda mrefu, kinyume na matakwa ya sheria.
Post a Comment