Kikosi
Kazi cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam cha kuzuia wizi wa
magari kimeendelea na kazi ya kudhibiti vitendo hivyo kwa kumkamata
Padri wa Kanisa Katoliki Sumbawanga Demestrious Apolinary kwa tuhuma za
kuhusika na ununuzi wa gari ya wizi.
Kamishna
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamanda Simon Sirro amesema
mnamo Novemba, 11 baada ya padri huyo kununua gari aina ya Toyota
L/cruiser T616 DCH mali ya Joseph Kayawaya lililoripotiwa kuibiwa Dar es
Salaam na nyaraka za kughushi na kuuzwa jijini Arusha.
Amesema
padri huyo anafanyiwa mahojiano na kwamba upelelezi utakapokamilika
atapelekwa mahakamani ili kuona kama ni mnunuzi asiye na hatia au
alishiriki kwa namna moja au nyingine katika wizi huo.
Kamanda
Sirro amesema pia Jeshi la Polisi linashikilia watuhumiwa wengine wanne
aliowataja kwa majina ya Aman Dickson, Exaud Martin, Rashid Haruna na
Mzee Nasibu kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa magari katika matukio
mawili tofauti.
Katika
tukio lingine, Kamanda Sirro amesema Jeshi la Polisi linashikilia
majambazi watano na vifaa mbalimbali walivyopora maeneo ya Tuwangoma
mtaa wa Masaki, Mbagala.
Post a Comment