Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi maarufu kama Mahakama ya Ufisadi imetupilia mbali pingamizi lililowekwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuhusu mamlaka iliyonayo katika kutoa dhamana kwa washtakiwa wa makosa ya rushwa.
Uamuzi
huo ulitolewa jana na Jaji Mfawidhi wa mahakama hiyo Rehema Mkuye
aliyesikiliza pingamizi la DPP dhidi ya maombi ya dhamana
yaliyowasilishwa na washtakiwa wawili wa kesi ya Uhujumu Uchumi,
wanaokabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Washtakiwa hao ni Mtanzania, Jeremiah Madar Kerenge (40) pamoja na Fu
Chang Feng (50), raia wa China, na Ally Damji Raza (34) raia wa India,
ambao wanadaiwa kukutwa na nyavu haramu za kuvulia samaki zenye thamani
ya jumla ya Sh22, 978,750,000.
Kerenge
na Raza waliwasilisha maombi ya dhamana katika Mahakama Kuu Divisheni
ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, lakini DPP aliweka pingamizi
akidai maombi hayo yamefunguliwa kwenye mahakama isiyo sahihi.
Wakati wa usikilizwaji wa pingamizi hilo Novemba 3, DPP kupitia kwa Wakili wa Serikali Mkuu (PSA) Vitalis Timon alifafanua kuwa sheria inataka maombi hayo yafunguliwe Mahakama Kuu na siyo katika Mahakama ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Hata
hivyo, katika uamuzi wake jana, mahakama hiyo ilitupilia mbali
pingamizi hilo la DPP na ikasema kuwa ina uwezo na kwamba mahakamani
hapo ndipo mahali sahihi pa kufungua maombi ya dhamana kwa washtakiwa
wote wa kesi za rushwa na uhujumu uchumi.
Kuhusu
kifungu cha 29 (4) (d) cha Sheria ya Makosa ya Uhujumu Uchumi
kinachoonyesha kuwa Mahakama Kuu ya kawaida ndio yenye mamlaka ya kutoa
dhamana kwa washtakiwa wa rushwa au uhujumu uchumi, Jaji Mkuye alisema
kuwa kuna makosa.
Alifafanua
kuwa kinachoonekana katika kifungu hicho ni usahaulifu tu wa Bunge na
kwamba nacho kilipaswa kufanyiwa marekebisho, kitamke kuwa maombi ya
dhamana katika kesi ya rushwa na uhujumu uchumi, lazima yafunguliwe
katika Divesheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
Alisema
kuwa kwa kuwa divisheni hiyo ina ofisi katika kila Kanda ya Mahakama
Kuu, ambako pia tayari kuna majaji maalumu walioteuliwa kushughulikia
kesi na maombi ya dhamana ya kesi za rushwa na uhujumu uchumi, hivyo
hakuna hofu yoyote ya mlundikano wa wananchi kusubiria maombi yao.
Wakati
wa usikilizwaji wa pingamizi hilo Novemba 3, Wakili Vitalis alidai kuwa
mahakama hiyo inakuwa na uwezo wa kutoa dhamana pale tu ambapo kesi ya
msingi inakuwa tayari imeshafunguliwa kwenye mahakama hiyo.
Hata
hivyo, wakili wa washtakiwa hao, Roman Lamwai alipinga hoja hizo akidai
kuwa mahakama hiyo ndio mahali sahihi kwa mujibu wa tafsri ya Sheria ya
Uhujumu Uchumi kama ilivyofanyiwa marekebisho.
Alisisitiza
kuwa hata ukubwa wa kiwango cha pesa katika hati ya mashtaka kwenye
kesi hiyo ni lazima maombi hayo yafunguliwe katika mahakama hiyo ambavyo
ndio yenye jukumu la kusikiliza na kuamua kesi za Rushwa na Uhujumu
Uchumi.
Baada
ya Mahakama kutupilia mbali pingamizi hilo, iliendelea kusikiliza
maombi ya dhamana ambapo Wakili Lamwai aliieleza mahakama kuwa mashtaka
yanayowakabili washtakiwa hao yanadhaminika na kwamba wote wako tayari
kutekeleza masharti ya dhamana.
Lamwai alidai kuwa mtoa maombi wa kwanza (Kerenge) ana mke ambaye ni mjamzito hivyo anahitaji kuwa naye karibu kumhudumia.
Kuhusu mtoa maombi wa pili (Raza), alidai kuwa mashtaka mawili yote yanayomkabili hayaangukii kwenye sheria ya Uhujumu uchumi, lakini kwa kuwa yameambatanishwa kwenye kesi ya uhujumu uchumi basi dhamana yake ilikuwa vigumu katika mahakama ya chini.

Aliongeza
kuwa yeye ni mfanyabiashara anayefanya biashara zake Dar es Salaam
ambako pia ndiko aliko na makazi yake ya kudumu hivyo hawezi kuruka
dhamana.
Akijibu
hoja za maombi hayo, Wakili Timon alidai kuwa baada ya pingamizi lao
kutupiliwa mbali, hawana pingamizi kuhusu dhamana, kwa kuwa mashtaka
yanayowakabili yanadhaminika na pia dhamana ni haki yao.
Hata
hivyo aliikumbusha mahakama kuwa wakati wa kutoa dhamana izingatie
kifungu cha 36 (5) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi kama ilivyofanyiwa
marekebisho mwaka 2016.
Kwamba kwa mujibu wa kifungu hicho, watoa maombi wanalazimika kuwasilisha mahakamani pesa taslimu au hati ya mali yenye thamani sawa na nusu ya pesa inayotajwa kwenye hati ya mashtaka, kwa utaratibu wa kanuni ya kugawana au kuchangia wote kiwango hicho cha pesa.

ya kusikiliza hoja za kila upande, Jaji Mkuye aliahirisha shauri hilo
hadi kesho atakapotoa uamuzi wa dhamana kwa washtakiwa hao.
Katika kesi ya msingi namba 45 ya mwaka 2016, inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa wa Mahakama ya Kisutu, inadaiwa walikutwa na nyavu ambazo zimepigwa marufuku kutumika wala kuhifadhiwa nchini zenye thamani ya jumla ya Sh22, 978,750,000.

Post a Comment