Siku
kadhaa baada ya utabiri wa TB Joshua kuwa Hillary Clinton angeshinda
urais wa Marekani kuwa tofauti, hatimaye mhubiri huyo maarufu wa Nigeria
ametoa ufafanuzi kuhusu kilichotokea.
Awali,
TB Joshua aliwaambia waumini wake kuwa aliona ndotoni kuwa Rais wa
Marekani atakayechaguliwa atakuwa mwanamke na kwamba atakumbwa na
changamoto nyingi ikiwemo jaribio la kutaka kumuondoa madarakani kwa
kura za kutokuwa na imani naye.
Mhubiri
huyo ametumia ukurasa wake wa Facebook na Twitter kuutetea utabiri wake
akidai kuwa Clinton alishinda kupitia kura za jumla, kwa kupata kura
nyingi zaidi ya Donald Trump.
“Tumeona
matokeo ya uchaguzi wa Marekani. Kwa kusoma, utagundua kuwa
[utabiri]ule ulikuwa kuhusu kura za jumla (popular votes), kura za
wamarekani wengi,” unasomeka ujumbe wa TB Joshua.
“Katika
hali hii, tunahitaji roho ya kinabii kutambua au kujua unabii. Viwango
vyetu ni tofauti. Hatuko kwenye viwango sawa. Tunaweza kuwa na makanisa
makubwa, kengele kubwa, na shughuli zote ambazo ni nzuri kwa viwango vya
kibidamu lakini uwezo wa binadamu una kikomo,” aliongeza.
Alitumia
pia Biblia Takatifu kuupa nguvu utetezi wake, akitaja maandiko ya 1
Wakorinto 1: 25, “Maana kinachoonekana kuwa ni upumbavu wa Mungu, kina
busara zaidi kuliko hekima ya binadamu; na kinachoonekana kuwa ni
udhaifu wa Mungu, kina nguvu zaidi kuliko nguvu za binadamu.”
Clinton
alishinda kwa kupata kura nyingi zaidi za Wamarekani (popular votes)
lakini alishindwa katika kura za majimbo muhimu (electoral votes).
Mgombea wa Republican ambaye tafiti nyingi hazikumpa nafasi, alishinda
uchaguzi huo na kuishangaza dunia.
Trump anatarajiwa kuapishwa rasmi kuwa Rais wa Marekani, Januari mwakani.
Post a Comment