ACP Advera Bulimba
Jeshi la Polisi nchini Tanzania limewapiga marufuku wamiliki wa
nyumba za starehe kuendekeza tamaa ya fedha kwa kujaza watu kupita kiasi
na kuwataka wazingatie uhalali wa matumizi ya kumbi zao na uwezo wa
kumbi hizo katika kipindi cha sikukuu.
Taarifa hiyo imesema kuwa ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine yote ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya ya watu.
Aidha jeshi hilo limetoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini na kuchukua hatua stahiki za haraka kwa kutoa taarifa kupitia kwa makamanda wa polisi wa miko pindi wanapoona viashiria vyovyote vya uhalifu.
Pia amewataka wazazi kuwa makini na watoto wao ili kuepuka upotevu wa watoto, ajali na matukio mengine yanayoweza kusababisha madhara.
Post a Comment