Michuano
ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON 2017) imeanza usiku wa jana kwa
kushuhudia sare mbili ikiwemo ya mwenyeji Gabon ambaye amelazimishwa
sare ya bao 1-1 na Guinea Bissau katika mchezo wa ufunguzi
Guinea Bissau walisawazisha bao la Aubameyang lililofungwa dakika ya 51 kunako dakika ya 89 kupitia Soares
Katika mchezo wa pili, Cameroon pia imelazimishwa sare ya bao 1-1 na Burkina Faso.
Leo
zinapigwa mechi mbili ya kundi B, ambapo saa 1:00 jioni Algeria
inakipiga na Zimbabwe huku Tunisia ikikipiga na Senegal saa 4:00 Usiku.
Post a Comment