0
Austria kupiga marufuku vazi la Burqa katika maeneo ya hadhara

Muungano unaotawala nchini Austria umekubali kupiga marufuku vazi la kiislamu la Burqa katika maeneo ya hadhara kama vile mahakama na shule.

Pia unaangazia marufuku ya jumla ya vazi la hijab pamoja na lile la ishara nyengine za dini.

Mikakati hiyo inaonekana kama jaribio la kukabiliana na umaarufu wa chama cha mrengo wa kulia cha Freedom Party ambacho mgombea wake alipoteza kwa uchache wa kura katika uchaguzi wa urais wa mwezi uliopita.

Muungano wa msimamo wa kati nusra uvunjike wiki iliopita kufuatia mgogoro wa majadiliano kuhusu mwelekeo wa serikali katika siku zijazo.

Akitoa mpango huo wa marekebisho, muungano huo ulitoa maelezo mawili kuhusu marufuku hiyo ya mavazi ya niqab na burqa.

''Tunaunga mkono jamii ilio wazi pamoja na mawasiliano yalio na uwazi.Hivyobasi vazi linalofunika uso mzima linaweka kizuizi katika kuafikia hilo na hivyobasi litapigwa marufuku'', ulisema.

Takriban wanawake 150 huvaa vazi la Niqab nchini Austria lakini maafisa wa utalii wanahofia kwamba mikakati hiyo itawazuia wageni kutoka eneo la mashariki ya kati.

Post a Comment

 
Top