0
Mchungaji Ambilikile Mwasapile 

Ngorongoro. Unamkumbuka yule Babu wa Samunge au Loliondo? Jina lake halisi anaitwa Ambilikile Mwasapile. Babu huyo pia ni mchungaji.

Mchungaji Mwasapile bado yupo na shughuli zake za kutoa kikombe cha dawa anayodai inatibu magonjwa  yote yanayomkabili binadamu.

Hata hivyo, baada ya ukimya wa muda mrefu babu ameibuka na kuitaka kwa mara nyingine Serikali kuboresha miundombinu ya Loliondo kwa kuwa kuna mambo makubwa yanakuja kutokana na maono anayoonyeshwa. Akizungumza nyumbani kwake katika Kijiji cha Samunge, Tarafa ya Sale jana, Mchungaji Mwasapile alisema watu waliokuwa wanakwenda kwa wingi miaka iliyopita wamepungua sana na sababu ni kuwa idadi kubwa ya walipokea uponyaji wakati huo.

Mchungaji huyo mstaafu alisema wito anaoutoa kwa Serikali kuboresha miundombinu unatokana na mambo makubwa anayoonyeshwa yatakayokuja wakati ambao Mungu ameupanga.

Post a Comment

 
Top