THE CIVIC UNITED FRONT
CUF – Chama cha Wananchi
CUF – Chama cha Wananchi hakina sababu ya kumjibu Mtatiro na Genge lake,
bali kwa kua kumeibuliwa hoja inayohusu Viongozi halali wa Cuf, tunaona
Kuna haja ya kutoa ufafanuzi Kuhusu Jambo hili.
Chama cha Wananchi kinaongozwa na Utaratibu wake wa Kikatiba. Kwa hivyo
anaejiona kua ni Kiongozi wa Kitaifa wa Chama hiki ni vyema aje kwenye
Vikao vya Chama ili aweze kupata ufafanuzi wa hoja hii badala ya
kulalama kwenye Vyombo vya Habari. Katibu Mkuu wa Chama hiki ni Maalim
Seif Shariff Hamad na Mwenyekiti wa Chama hiki ni Prof Ibrahim Haruna
Lipumba. Ni kweli Cuf tumeomba Fedha zetu za Ruzuku ili ziweze
kutusaidia kwenye Uchaguzi huu wa Madiwani katika Kata 20 kwa upande wa
Tanzania Bara.
Ni vyema Watanzania wakafahamu kwamba kupitia kwa Shaweji Mketo, upande
wa Maalim Seif Shariff Hamad umetamka bayana kwamba haujasimamisha
Mgombea kwenye Kata yoyote katika Uchaguzi huu Mdogo unaotarajiwa
kufanyika January 22 Mwaka huu. Upande wa Bara Cuf imesimamisha Wagombea
kwenye Kata 14 kati ya Kata 20 zinazopaswa kurudia Uchaguzi.
CUF, Chama cha Wananchi upande wa Bara hatuwezi kuacha kusimamisha
Wagombea na kuamua kuunga Mkono Wagombea wa Chadema kama ilivyoelekezwa
na Katibu Mkuu tu, kupitia Shaweji Mketo. Kuhusu suala la Ruzuku ni
kweli kwamba Ofisi ya Msajili ilisimamisha Ruzuku kwakua, ilipokea
Malalamiko toka kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa na baadhi ya viongozi
Kuhusu kuvurugika kwa Mkutano huo kulikotokana na ukiukwaji wa Katiba ya
Cuf. Kwa sasa Mgogoro huo haupo, kwa hivyo sisi tumeomba Ruzuku hiyo
ambayo ni Haki yetu kama Chama, na kwakua Mgogoro umekwisha, Msajili
hana sababu ya kuendelea kusimamisha Ruzuku hiyo.
Ni kweli pesa hizo zimeingizwa kwenye akaunti ya Chama na zinatumika
kwenye Shughuli za Chama ikiwa ni pamoja na Uchaguzi wa Udiwani
unaorudiwa katika Kata 20 hapa Tanzania Bara. Lakini Maalim Seif Shariff
Hamad na Genge lake kama wakweli, basi waeleze pia kua Mwezi October
wametoa Milioni 86 kwenye akaunti ya NBC bila ya kuhusisha upande wa
pili wala kumuhusisha Naibu Katibu Mkuu Bara Magdalena Sakaya ambae ni
Mmoja ya watia saini kwenye akaunti hiyo.
Kwa upande wetu hatukuona shida pamoja na kutojuliswhwa kwakua tunajua
kua pesa hizo zinaenda kwenye Uchaguzi wa Jimbo la Dimani. Mtatiro
hawezi kuyafahamu haya kwakua si Kiongozi wa Chama hiki.
Tunawataka Wanacuf kupuuza kelele hizo kwakuwa zinalenga kuwatoa kwenye
Harakati za kutafuta ushindi wa Chama na Wagombea wetu kwenye Uchaguzi
huu wa Madiwani. Si kosa na wala hakuna shida yoyote kwa Ofisi ya
Msajili kutupatia Ruzuku hiyo na kama Kuna Kiongozi yeyote ambae yupo
kwa mujibu wa Katiba yetu na anataka kujua Matumizi yake basi asubiri
Vikao vya Chama.
Abdul Kambaya
Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
HAKI SAWA KWA WOTE
Post a Comment