Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) linawaarifu wateja
wake na umma kuwa leo Ijumaa saa 2:30 asubuhi kumetokea hitilafu katika
njia za usafirishaji umeme kutoka mkoani Morogoro - Kidatu na Morogoro -
Kinyerezi iliyisababisha mikoa iliyo unganishwa katika gridi ya Taifa
kukosa umeme isipokuwa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Taaria iliyotolewa na ofisi ya uhusiano ya Tanesco imesema jitihada zimefanyika kutatua hitilafu hiyo na hivyo kupelekea baadhi ya mikoa kuanza kupata huduma ya umeme.
Mikoa hiyo ni Singida, Dodoma na Iringa.
“Mafundi wanaendelea na jitihada zaidi kuhakikisha umeme unarejea katika hali yake ya kawaida katika Mikoa iliyo salia.”

Post a Comment