Bado
kazi ya uokoaji wa watu 14 waliofukiwa na kifusi katika Mgodi wa
Dhahabu wa Kampuni ya RZ Union Mining Ltd uliopo Kata ya Nyarugusu
mkoani Geita inaendelea, na hadi jana waokoaji hawajafanikiwa kuokoa mtu
yoyote.
Pamoja na juhudi hizo za uokoaji, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ezekiel Kyunga amesema kuwa ana imani watu hao wataokolewa wakiwa hai.
Amesema
kuwa jana imefanyika kazi kubwa ya kuchimba kifusi ili kutafuta njia ya
kuwafikia waathirika huku mipira zaidi ya Oxygen ikiingizwa chini ya
mgodi waliko watu hao ili kuwaongezea hewa.
Aidha,
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Latson Mponjoli amesema juhudi za
uokoaji zinaendelea kwa ushirikiano wa vikosi vya uokoaji vya Kampuni ya
Geita Gold Mine (GCM), Jeshi la Zimamoto na Polisi pamoja na kikosi cha
ukoaji cha Sekta ya Madini.
Amesema hali ni shwari katika eneo hilo na wana matumaini ya kuwafikia watu hao wakiwa hai.
Pia,
Kampuni inayoendesha mgodi huo imesema kutokana na kitabu cha orodha ya
watu wanaojiandikisha kuingia mgodini, kuna majina ya Watanzania 12 na
Mchina mmoja waliofukiwa kifusini. Ilielezwa kuwa watu pia
waliomshuhudia Mtanzania mmoja akingia mgodini humo bila kujiandikisha
na hivyo kufanya waliofukiwa kufikia 14.
Watanzania
13 na raia mmoja wa China walifukiwa na kifusi juzi usiku baada ya
udongo kuziba mlango waliokuwa wakitumia kuingia na kutoka.
Post a Comment