Madaktari watatu wa hospitali ya Ngudu wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza
wamekamatwa na polisi kwa amri ya mkuu wa wilaya hiyo Mhandisi Mtemi
Msafiri kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za rushwa na kughushi saini za
wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo.
Madaktari waliokamatwa na polisi na kunaswa na kamera ya ITV ni Dk. Gaspar Luziga ambaye ni mratibu wa chanjo wilayani Kwimba, Dk. Esther Kanyasu wa kitengo cha mionzi na Dk. Bethord Nchemba wa kitengo cha upasuaji.
Dk. Luziga anatuhumiwa kughushi saini na kujipatia kiasi cha shilingi milioni 9 kwa njia za udanganyifu, pesa ambayo ingetumika kwa ajili ya chanjo ya mama na mtoto, ambapo Dk. Nchemba anatuhumiwa kumfanyia upasuaji mgonjwa ambaye jina lake tunalihifadhi na kujipatia kiasi cha shilingi laki moja, huku dk. Kanyasu akituhumiwa kuomba rushwa kutoka kwa mgonjwa ili ampatie matibabu.
Mapema, muuguzi mfawidhi wa hospitali ya Ngudu Catherine Donald ameeleza baadhi ya changamoto anazokutana nazo hasa pale anaposimamia suala la maadili kwa wauguzi wa hospitali hiyo na wagonjwa kutotendewa haki.
Baadhi ya wauguzi na watumishi wa hospitali hiyo wamelalamikia mazingira magumu ya kazi yanayosababishwa na ukosefu wa vifaa tiba na vitendea kazi, hali inayokwamisha utoaji wa huduma bora za afya kwa wagonjwa.

Post a Comment