Muigizaji wa filamu za vichekesho nchini Amri Athumani maarufu kama
'Mzee Majuto' ambaye mwaka jana aliwahi kutangaza kuacha uigizaji na
kumrudia Mungu amefunguka na kusema kuwa ataendelea kuigiza mpaka
anakufa kwa sababu uigizaji upo kwenye damu.
Mzee Majuto
Akiongea na EATV Mzee Majuto alisema kuwa yeye hawezi kukubali kuona
fani inachezewa chezewa na watoto hivyo ataendelea kuigiza mpaka siku
atakayokufa kwa sababu uwezo wake ni wa hali ya juu kwenye kuandika na
kuigiza.
"Kuigiza kwangu ni kama maradhi vile hivyo sidhani kama naweza kuacha,
siwezi kukaa pembeni sanaa ikawa inachezewa na watoto sitaki kabisa
nasema hivi mimi nitaendelea kuigiza mpaka nakufa". Mzee Majuto
Post a Comment