Klabu
ya KRC Genk baada ya kuumia mshambuliaji wao Nikolaos Karelis ambaye
alikuwa anashindania namba na mtanzania Mbwana Samatta atangazwe kuwa
atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi 8 hadi 9 baada ya kupata
jeraha la goti la kushoto alilolipata wakati wa mchezo dhidi ya KAA Gent
December 27.
Katika kipindi hiki cha usajili January 10 2017 klabu ya KRC Genk
imetangaza kufanya usajili wa mshambuliaji Jose Naranjo kutokea Celta
Vigo ya Hispania, mchezaji huyo anakuja kumpa changamoto mpya Mtanzania
Mbwana Samatta kuendelea kupambania namba ya kucheza na Naranjo katika
kipindi ambacho Karelis atakuwa nje.
Mshambuliaji Nikolaos Karelis ambaye kwasasa ni majeruhi
Mchezaji Jose Naranjo amesajiliwa kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu
wakuitumikia klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji akitokea Celta Vigo ya
Hispania. Naranjo ambaye ana umri wa miaka 22.
Mchezaji Jose Naranjo ambaye amesajili na KRC Genk
Post a Comment