0
 Timbulo
Msanii Timbulo anayetamba hivi sasa katika bongo fleva na ngoma yake ya 'Usisahau', amefunguka na kusema kuwa baadhi ya wasanii waliokuwa wakikwepa na kumtolea nje kushirikiana naye katika muziki, hivi sasa wanamtafuta wao
Timbulo ametoa siri hiyo kupitia eNewz na kukumbushia maumivu aliyoyapa mara baada ya kutoswa na wasanii Malaika na Vanessa pindi alipohitaji kufanya nao kazi kwa nyakati tofauti.

Amesema kinachofanya hivi sasa wamtafute ni kufanya vizuri kwa ngoma yake mpya 'Usisahau ' aliyomshirikisha Baraka The Prince na kueleza sababu ya kumtumia Baraka katika ngoma hiyo badala ya msanii wa kike.

“Ni ngoma ambayo Baraka aliisikia na kutaka kuingiza sauti yake tofauti na dada zetu ilipofika time natafuta sauti ya mwanamke nilisumbuka, vitu vingi sana vilitembea, mara wengine wanasema kuwa hawanijui kina Vannesa wengine kufanya audio mara video mtu kazingua kwa hiyo mimi ninachokiona ni ulevi wa madaraka labda kwa sababu mtu yuko kwenye peak" Alisema Timbulo

Ameendelea kusema "Msanii ukikaa kimya unaona watu waliokuwa wanakutafuta wanapungua na inafikia hatua ukimcheki mtu aliyekuwa anakupigia simu na yeye anavimba lakini ukirudi tu kidogo, zile simu ambazo zilikuwa zikiku 'ignore' ndizo zinakutafuta”
Vanessa Mdee

Pia alimalizia kwa kumpa salamu Vanesa na kusema kuwa yeye ndiyo Timbulo na ngoma ya 'Usisahau' ndiyo yake

Timbulo ni mmoja kati ya wasanii ambao mwaka 2016 haukuwa mzuri sana kwake wakari alipotaka kurudi kwenye game baada ya kukutana na changamoto nyingi sana katika muziki wake ambapo aliwahi kutoa ngoma na ndani ya ngoma yake hiyo alimshirikisha Malaika lakini siku ambayo alihitaji kufanya video na msanii huyo hakutokea na kushindwa kufanya video hiyo,

Pia mwanadada Vanessa Mdee naye aliwahi kusema kuwa hamfahamu msanii huyo pale ambapo msanii huyo alipompigia simu na kumuomba afanye naye 'collabo' Vanessa alisema kuwa hamfahamu kitendo ambacho kilimuumiza sana Timbulo.

Post a Comment

 
Top