0
Aliyekuwa mchezaji wa West Ham Dimitri PayetAliyekuwa mchezaji wa West Ham Dimitri Payet
Wachezaji wa klabu ya West Ham walitaka Dimitri Payet kuondoka katika klabu hiyo kabla ya kuelekea Mersaille ,kulingana na mwenyekiti mwenza wa klabu hiyo David Sullivan.
Mshambuliaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29 alijiunga tena na klabu yake ya zamani kwa kitita cha pauni milioni 25 baada ya kudaiwa kukataa kuichezea West Ham kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita.
''Kwa kweli hatukutaka aondoke lakini huwezi kwenda kinyume na umoja wa timu'' ,sullivan aliambia BBC.
Sullivan alisema kuwa Payet aliamua kutochukua mshahara wake wa Januari.
''Payet hakuzungumza na mtu kwa wiki sita.Amekataa kuzungumza na mtu yeyote katika timu'',alisema Sullivan.
Payet alijiunga na West Ham mwezi Juni 2015.

Post a Comment

 
Top