SERIKALI imetangaza vita dhidi ya watu wanaouza ardhi na wamiliki wa
nyumba wanaopangisha kwa bei ya juu, huku ikisisitiza kuwa inaandaa sera
itakayowadhibiti kwa kuweka bei elekezi.
Akizungumza katika ziara ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii katika Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA), Naibu Waziri wa wizara hiyo, Angelina Mabula, alisema kumekuwa na uuzaji holela wa viwanja kwa bei kubwa ingawa baadhi ya maeneo hayo hayana miundombinu mizuri ikiwamo ya barabara, umeme na maji.
Mabula alisema kupitia hotuba ya mwaka jana ya bajeti, serikali ilibainisha dhamira yake ya kuanzisha sera mahususi itakayopanga bei ya kuuza viwanja katika maeneo mbalimbali nchini.
Post a Comment