0
Wananchi walioguswa na mradi wa uboreshwaji wa miundombinu ikiwemo barabara, mifereji, taa za barabarani madaraja wilayani Temeke wamekubali kubomoa nyumba zao ili kupisha mradi huo utakaogharimu ya shilingi bilioni 266 fedha zilizotolewa kama mkopo kwa benki ya dunia.

Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo litakalopojengwa daraja kubwa la mita 800 litakalounganisha kata ya Kijichi na Tuangoma hadi wilaya ya Kigamboni ikiwa ni sehemu ya mradi huo mkuu wa wilaya ya Temeke Felix Lyaniva amesema daraja hilo litasaidia kuchochea uchumi na maendeleo ya wananchi wa Temeke.

Kwa upande wake mratibu wa mradi wa uboreshwaji wa miudnombinu manispaa ya Temeke Bw, Edward Haule amesema mradi huo unalenga kuijenga Dar es Salaam mpya ambapo manispaa ya Temeke imechangia shilingi bilioni 20 kwa ajili ya ulipaji wa fidia kwa wananchi.

Aidha pia mkuu wa wilaya hiyo alizungumza na baadhi ya wananchi walioguswa na mradi huo kata ya Kilungule Nzasa na Buza ili kujua kero zao juu ya mradi huo ambapo aliwahakikishia wote watalipwa fidia zao kisha akazindua kitabu cha mwongozo wa utendaji kazi wa kamati za utatuzi wa migogoro katika mradi huo (DMDP) kwavile mradi hauwezi kutekelezwa kukiwa na malalamiko ya wananchi ikiwa ni moja ya sharti la wafadhili waliotoa fedha hizo.

Post a Comment

 
Top