0
 Z Anto si wamchezo mchezo. Muimbaji huyo aliyewahi kufanya vizuri na wimbo wake ‘Binti Kiziwi’ amewaonesha mashabiki mafanikio anayoyapata nje ya muziki.

Kupitia mtandao wa Instagram, muimbaji huyo ameonyesha picha ya nyumba ambayo haijaisha na kudai kuwa huo ndio mjengo wake wa nne ambao anaujenga kwa sasa.

“Wiki mbili za mwaka 2017. House namba 4. Mwaka ndivyo tulivyouanza. #Thnxgod #njeyasanaa,” ameandika Z Anto katika picha hiyo hapo juu aliyoiweka katika mtandao huo.

Post a Comment

 
Top