Moshi. Polisi mkoani Kilimanjaro imemtaka dereva aliyesababisha ajali
katika eneo la Mwika Mawanjeni wilayani hapa na kusababisha vifo vya
watu wanane, akiwamo mwandishi wa habari, Arnold Swai (28) kujisalimisha
kituo cha polisi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema dereva huyo aliyefahamika kwa jina la James John mkazi wa Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, alikimbia baada ya kusababisha ajali juzi.
“Gari hilo lilifeli breki likiwa kwenye mteremko na kugonga gari aina ya Toyota lililokuwa likiendeshwa na Jackson Kimambo, ambaye ni mwandishi wa habari na mkazi wa Rau,” alisema Kamanda Mutafungwa.
Alisema dereva aliyekimbia alikuwa akiendesha gari aina ya Mitsubishi Fuso lililokuwa likitokea wilayani Rombo kwenda Himo likiwa limebeba magunia ya viazi.
Kamanda Mutafungwa alisema wanamshikilia mmiliki wa Fuso ili kutoa maelezo na kuisaidia polisi ili kumpata dereva aliyekimbia.

Post a Comment