0
Q Chillah

 Familia ya msanii wa bongo fleva Q Chilla wameamua kuingilia kati mkataba wa msanii huyo na kusema mkataba huo unamfanya aishi maisha magumu kiasi cha kushindwa kuchangia mambo yakifamilia.
Akiongea kupitia eNewz ya EATV, baba mdogo wa Q Chila amesema kwamba hofu juu ya mkataba ni kwamba haukuwa na ushahidi wowote kwa upande wa Q Chilla hali inayombana na kushindwa kuendelea kimaisha na kushindwa kuwa na  nyumba yake.

Amesema familia hiyo imeamua kumuandikia barua bosi wa Q Chillah ambaye ni QS Mhonda kumuomba kubadilisha sehemu mbalimbali ambazo zinambana sana kijana wao kiasi cha kumsababishia kurudi alipotoka jambo linaloweza kumvurugia maisha yake.

Post a Comment

 
Top