Taarifa kutoka Butiama kwenye Mkoa wa Mara leo ni kuhusu miili ya watu
wawili kupatikana February 14 2017 kwenye Mgodi wa Buhemba ambapo kwa
taarifa za awali watu 13 wameokolewa wakiwa wamejeruhiwa baada ya
kufukiwa ndani ya mgodi.
Kutoka kwenye eneo la tukio, Mkuu wa Wilaya ya Butiama Annarose Nyamubi
amesema “Ni kweli kabisa kwenye Wilaya ya Butiama Magunga ulipo mgodi wa
zamani wa dhahabu wa Buhemba shimo moja limefukiwa na kifusi saa 3
asubuhi”
“Mpaka saa 7 mchana tuliweza kuokoa watu 13 na wengine wanaendelea na
matibabu huku wengine wakiwa wameruhusiwa wako nyumbani, kuna Wachimbaji
wengine wanne bado wanatafutwa na idadi inaweza kuongezeka”
“Idadi inaweza kuongezeka kwasababu kuna Wachimbaji ambao huwa wanazamia
bila kujisajili majina yao kabla ya kuingia mgodini, wale ambao huwa
wanajisajili ndio rahisi kutambua rekodi zao… tunavyoendelea na zoezi” –
DC Annarose
Post a Comment