Utawala nchini Marekani umewasilisha rufaa ya kutaka kurejeshwa kwa
amri ya Rais Donald Trump ya kuwazuia raia wa mataifa saba ya waislamu
kusafiri hadi Marekani, baada ya mahakama kuipinga hapo awali.
Tangazo hilo linafuatia misururu kadhaa ya tweeter kutoka kwa Trump, ambapo anampinga jaji aliyetoa uamuzi huo, huku akionya kuwa watu wabaya na hatari, huenda wakamiminika hadi Marekani kutokana na uamuzi huo.
Mashirika makubwa ya usafiri wa ndege, yangali bado yanawakubalia raia
kutoka mataifa hayo husika, kuabiri ndege na kuingia Marekani.
Kumekuwepo na maandamano dhidi ya marufuku hiyo ya Trump huko
Washington, jimbo la Miami na miji mingine kadhaa ya Marekani, pamoja na
miji mingine mikuu ya bara Ulaya.

Post a Comment