WALIMU wa Shule ya Sekondari Bilele Manispaa ya Bukoba, wanalazimika
kuchangia vyoo na wanafunzi hali inayowaletea adha katika utendaji wao.
Mkuu wa shule hiyo, Ashura William, aliyasema hayo wakati akisoma taarifa fupi kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)wilayani Bukoba, Ashirafu Kazinja, aliyetembelea kukagua maendeleo shuleni hapo.
Ashura alisema sasa ni miezi mitatu tangu walimu hao 26 wa shule hiyo walipoanza kutumia vyoo vya wanafunzi baada ya vyoo vyao kuathiriwa na tetemeko la ardhi Septemba 10, mwaka jana.
Hata hivyo, Mkuu huyo wa shule alisema walipeleka taarifa za tatizo hilo kwa Ofisa Elimu Sekondari wa halmashauri hiyo kupitia Ofisi ya Mkurugenzi ambayo ilitoa mifuko 18 ya saruji pamoja na mabati manne ili kukarabati choo cha walimu.
Alisema baada ya kupokea vifaa hivyo vya ujenzi, ofisa huyo alimtaka apeleke bajeti ya ukarabati wa choo hicho ili kuingizwa katika awamu ya shule zinazotakiwa kukarabatiwa.
Hata hivyo, alisema baadaye waliambiwa wasubiri awamu ya tatu, lakini juzi tuliambiwa hakuna namna tena kwani kamati ya maafa ya mkoa imevunjwa," alisema Ashura.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Shule, athari kubwa iliyopo kwenye choo hicho ni kupasuka kwa kuta na kubomoka pembeni na makisio ya gharama za ukarabati yalikuwa ni Sh. milioni mbili.
Hata hivyo, alisema mkakati uliopo sasa ni kukaa na ofisi ya Mratibu Elimu Kata, Mtendaji wa Kata kutafuta njia za kurejesha miundombiu ya choo ili walimu waendelee kutumia vyoo vyao.
Akijibu hoja hizo, Mwenyekiti wa UVCCM alisema anatambua umuhinu wa choo hasa mazingira ya shule, hivyo miundombinu urudishwe haraka ili walimu waondokane na adha ya kuchangia choo na wanafunzi.
Kwa upande wake, Ofisa Elimu wa Shule za Sekondari Manispaa ya Bukoba Wandele Rwakatale, alisema ukarabati wa vyoo hivyo utafanyika hivi karibuni kwani Sh. milioni tisa kutoka Wizara ya Elimu, Tejonolojia na Mafunzo ya Ufundi, zimeshafika Halmashauri.

Post a Comment