0
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Bi. Margaret Mussai  pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeley ya Jinsia Bwana Julius Mbilinyi  akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani kughusu siku ya kimataifa ya kuzuia ukeketaji.

Masuala ya ukatili wa kijinsia ikiwemo ukeketaji yameendelea kuwa tatizo kwa taifa na ulimwengu mzima na ili kukabiliana na tatizo hili, kumekuwa na mwitikio mkubwa wa kimataifa na kitaifa katika kukabilana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Akiongea na vyombo vya Habari Jijini Dar es Salaam leo  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Watoto wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Margaret Mussai amesema Serikali inalaani na kukemea vikali ukatili kwani unadhalilisha na kunyanyasa hadhi na utu wa mwanamke na mtoto wa kike akisema jambo hili halikubaliki.

Aidha aliongeza kuwa ni lazima jitihada za makusudi zichukuliwe na wadau wote kuhakikisha kuwa tunashiriki kwa pamoja kuzuia na hatimaye kutokomeza ukatili wa kijinsia katika jamii zetu, hususan kuzua ukeketaji.




Post a Comment

 
Top