Dar es Salaam. Wako wanaofikiria kupumzisha magari yao kutokana
na mzigo mkubwa wa gharama za kuyatumia, na hasa bei ya mafuta ambayo
inaendelea kupanda, huku kipato kikiendelea kudumaa.
Baadhi wanaweza kuingia katika majaribu ya kununua petroli kwa bei rahisi mitaani wakati ubora wake umeshapunguzwa baada ya wauzaji kuichakachua kwa kuichanganya na mafuta ya taa na hivyo kuwa hatari kwa injini.
Wakati hali ya kiuchumi ikizidi kuwa ngumu kwa Watanzania wengi, ambao wanaona mkakati wa Serikali wa kubana matumizi umewaathiri, gazeti la Mwananchi linalo suluhisho la kukuwezesha uendelee kutumia gari lako katika mazingira hayo.
Wataalamu waliozungumza na mwandishi wetu wameeleza mbinu kadhaa za kumuwezesha mtumiaji gari kuepuka kutumia mafuta mengi wakati anapoliendesha na hivyo kujipunguzia mzigo wa gharama za mafuta.
Mbinu hizo zinahusisha kutembea wakati hakuna foleni; kwa safari ndefu, kutumia kiyoyozi; madereva kubadili hulka zao, matunzo na muundo wa gari na ubebaji wa mizigo mizito.

Post a Comment